Social Icons

Tuesday 10 April 2018

HERI YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA BLOGGER CATHBERT KAJUNA

Leo Aprili 10 ni siku ya kuzaliwa kwa Journalist/Photojournalist na Blogger Cathbert Angelo Kajuna mmiliki wa Kajunason Blog (www.kajunason.com) na Mwandishi/Mpigapicha wa MMG.


"Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunifikisha siku ya leo ya kuzaliwa kwangu, hakika yeye ni mwema maana amenivusha katika milima na mabonde na amekuwa akinifanyia mambo makubwa katika maisha yangu.

Pili nipende kutoa shukrani kwa familia yangu, ndugu jamaa na marafiki wote ambao mmekuwa bega kwa bega pale ambapo nimekuwa nikikwama mmekuwa mkinishika mkono na kunivusha hakika sina cha kuwalipa bali mwenyezi Mungu awaongezee busara, upendo na amani.

Tatu, kabisa nipende kutoa shukrani za pekee kwa Mke wangu, Mama yangu Mzazi, baadhi ya ndugu na marafiki ambao bila wao labda nisigekuwa hapa leo, nianze na Familia ya Kajuna Jr (Kennedy), Familia ya Michuzi Media Group ikiongozwa na Ankali Michuzi, Michuzi Jr na Othman hakika najivunia ukarimu na upendo wetu kwangu najivunia kuwa mmoja ya mwanafamilia, Familia ya Jackson Mmbando, rafiki zangu Seki David, Edwin David, Portnes, Mwesiga Kyaruzi, Shebby Mpondela, Franklin Alexander, Ally Jamal, Imani Ntila, James Jonathan na Dr. Heri Tungaraza. Wengine ni Raymond Maganga, Myoma Kapya - Chilala, Mike Mukunza, Muhidin Sufian, Bakari Kimwanga, John Bukuku, Abraham Mossi, Sylvia Mwehozi, Leah Mushi, Mary Masinda, Tiba  Josephat Lukaza, Ruben (Baba Countinho) na wale wote ambao nimekuwa nikishirikiana nao kwa namna moja au nyingine katika kusaka ugali wetu wa kila siku.

Mwisho, Shukrani za pekee ziwaendee wanachana wote Tanzania Bloggers Network (TBN) popote mlipo nawaomba tuendelee kushirikiana kwa pamoja, Umoja ni Nguvu.


No comments: